Waziri wa afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe ameeleza kusikitishwa na kitendo cha tabia mpya ya walevi nchini humo kuagiza soseji moja na bia mbili migahawani ili wapate nafasi ya kunywa na kulewa.

Hayo yamejiri baada ya serikali nchini kenya kupiga marufuku kufunguliwa kwa bar na kuruhusu maeneo yanayouza chakula kuwahudumia wanaohitaji vinywaji wakati wakisubiri chakula.

Kagwe amesema ” watu wamekuwa wanaenda kwenye migahawa na kuagiza soseji moja na bia mbili, wakimaliza wanahamia mgahawa mwingine na kuagiza tena soseji moja na bia mbili…wanafanya hivyo hadi wanalewa”

Wakati hayo yakijiri, zaidi ya watu 40 wametiwa mbaroni baada ya kukutwa wanakunywa pombe mchana ndani ya baa eneo la Umoja.

Uturuki: Tupo tayari kwa fainali Ligi Ya Mabingwa
Hersi Said amkataa Said Ndemla