Mfanyabiashara, mkazi wa Kijiji cha Kikweta Kata ya Lumemo Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, Petronila Ngurukila amemzawadiwa Pikipiki Polisi Kata ya Lumemo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Edwin Kipimo aliyekuwa akitumia usafiri wa baiskeli kutoa elimu kwa Wananchi juu usalama wa raia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa Polisi, Alex Mkama amemshukuru Mwananchi huyo kwa msaada huo na kumpongeza Mkaguzi Kipimo kwa kufanya kazi inayoigusa jamii kiasi cha kupelekea kupata msaada huo.

Awali akikabudhi msaada huo, Petronela alieleza kuwa, “kuna tukio moja lilikuwa gumu sana katika Kijiji ninachoishi nikampigia simu Polisi Kata kwa ajili ya kutupa msaada lakini alichelewa kufika.”

Alisema, “nikamuuliza vipi mbona hufiki akasema nipo hapa kwenye msitu nakuja, alipofika nikamuona anatokea na Baiskeli, nikamuuliza Afande usafiri uko wapi akajibu huu ndio usafiri wangu, nilisikitika sana nakuona kuna umuhimu wa kuwasaidia Polisi wetu.”

Naye mlengwa wa msaada huo, Afande Kipimo alimshukuru Mwananchi huyo kwa msaada wa Pikipiki hiyo na kuahidi kuitunza ili kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.

Matibabu ya Waraibu: Asilimia 90 ya wanaojitokeza ni Wanaume
Ajali: Basi lagongana na Lori, wawili wafariki