Kiungo wa klabu ya New York City FC ya Marekani, muitaliano Andrea Pirlo ametangaza kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 38.
Tangu ahamie katika klabu ya New York City Fc kiungo huyo wa Italia amekuwa hayuko vizuri uwanjani huku akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara na amekiri kwamba mwili wake umechoka na anahitaji kupumzika.
Mkataba wa Pirlo unamalizika mwezi December mwaka huu na mkongwe huyo amesema hatasaini mkataba mwingine na amesema kwamba wakati umefika kuwaachia nafasi vijana.
-
Hii ni habari mbaya kwa mashabiki wa Manchester United
-
Bayern Munich yamrejesha Jupp Heynckes
-
Kocha wa zamani wa Mwadui FC kurejea kuinoa timu hiyo
Kiungo huyo mkali wa kupiga pasi amecheza kwa kiwango cha juu katika vilabu vikubwa nchini Italia ikiwa ni pamoja na klabu za Juventus, Ac Millan na Inter Millan.
Pirlo ameshinda ubingwa wa nchini Italia Serie A mara 6 huku pia akishinda Champions League mara mbili na alikuwa mhimili mkubwa wakati Italia wakibeba kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.