Rapa Nelly ambaye alikamatwa Jumamosi iliyopita akituhumiwa kumbaka mwanamke mmoja kwenye gari lake ameeleza jinsi ambavyo anajipanga kuanika kile alichokiita ‘uongo mkavu’ wa mwanamke huyo.

Katika madai hayo, Mwanamke huyo ameeleza kuwa timu ya Nelly ilimualika kwenye hafla yao na kisha akaondoka na gari na watu wa rapa huyo ambao walimuhamishia kwenye gari lake (Nelly).

Amesema akiwa kwenye gari hilo, Nelly alimlazimisha kufanya naye mapenzi tena bila kutumia kinga, kitu ambacho msichana huyo alikipinga. Hata hivyo, anadai Nelly alimlazimisha na kumtaka ‘kufunga mdomo wake’ na kisha akatekeleza matakwa yake bila kinga.

Mwanamke huyo ameeleza kuwa baada ya kumfanyia kitendo hicho, Nelly alimpa fedha lakini alikataa. Anasema Nelly alimfukuza kwenye gari lake na kumrushia kitita cha fedha kiasi cha dola za kimarekani 100 ($100).

Timu ya Nelly imekanusha vikali tuhuma hizo na kueleza kuwa imejipanga kuuanika uongo wake.

Mwanasheria wa Nelly, Scott Rosenblum amesema kambi yao imemuajiri mpelelezi binafsi ambaye atafuatilia na kuweka wazi kilichofanyika katika tukio hilo, kwa kutumia teknolojia.

Rosenblum alisema kuwa mwanamke huyo anajitahidi kutafuta umaarufu na fedha kupitia uongo ambao ameupika kama mwandishi wa vitabu vya kutunga.

“Anatumia tuhuma hatari, za kufoji na kutunga ili kukamilisha lengo lake la kujipatia fedha na umaarufu,” alisema.

Nelly alikamatwa Jumamosi iliyopita kwa tuhuma hizo na aliachiwa baadae kwa dhamana.

Andrea Pirlo atangaza kutundika daruga
Video: Sitaki kuzozana na familia ya Lissu - IGP Sirro, Angellah Kairuki atikisa kila kona