Wakati ligi kuu ya soka Tanzania bara ikisimama kupisha michuano ya kombe la Challenge itakayoanza kutimua vumbi lake mwishoni mwa juma hili nchini Kenya, msimamo wa wafungaji katika ligi hiyo bado unaongozwa na mshambuliaji kutoka Uganda na klabu ya Simba Emmanuel Okwi.

Okwi ambaye aliosa michezo ya mzunguuko wa 10 na 11, amefunga mabao manane akifuatiwa na mchezaji mwingine kutoka nje ya Tanzania Obrey Chilwa (Zambia) wa Young Africans.

Ifuatayo ni orodha wa wafungaji kumi bora wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2017/18, ambayo inaelekea mzunguuko wa 12.

  1. Emanuel Okwi (8) – Simba
  2. Obrey Chirwa (6) – Young Africans
  3. Mohammed Rashidi (6) – Prisons
  4. Ibrahim Ajib (5) – Young Africans
  5. Shiza Kichuya (5) – Simba
  6. Asante Kwasi (5) – Lipuli
  7. Habibu Kiyombo (5) – Mbao FC
  8. Eliudi Ambokile (4) – Mbeya City
  9. Marcel Kaheza (4) – Majimaji
  10. Mbaraka Yusuph (3) – Azam FC

Ratiba ya kombe la Mapinduzi 2018 yaanikwa hadharani
Wenger: Sanchez, Ozil hawaondoki Januari