Baada ya kikosi cha Yanga kupoteza mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya Zesco United sasa nguvu zao wanazielekeza kwenye Kombe la Shirikisho.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa haikuwa malengo ya Yanga kufikia hatua hiyo ila ni matokeo haina budi kuyapokea.
“Kwa sasa sisi ni wa kimataifa, kushindwa kwetu kutinga hatua ya makundi haina maana ya mwisho wa mbio kimataifa bali tunaingia kwenye Kombe la Shirikisho huko tutapambana.
“Shukrani kwa mashabiki kwa ‘sapoti’ kubwa na Yanga tumeonesha maana ya kuwa wa kimataifa tumetoka kulia tumeingia upande wa kushoto,” amesema Nugaz
Yanga ilitolewa na Zesco kwenye hatua ya kwanza ya Ligi ya mabingwa kwa jumla ya mabao 3-2 hivyo wamefungasha virago kwenye michuano ya Ligi hiyo na kutupwa kwenye Kombe la Shirikisho.