Daktari justice Authur kutoka Afrika kusini ameshauri kuhusu matumizi ya simu ya mkononi (Smart Phone) nyakati za usiku hasa taa zikiwa zimezimwa ambapo amesema tabia hiyo inaweza kusababisha matatizo makubwa.

Naye Profesa Li Li, kiongozi wa hospitali ya macho huko Singapore amesema mionzi ya simu inayoingia ya moja kwa moja kwenye macho kwa zaidi ya dk 30 na kuendelea inaweza kusababisha mpangilio na mbadiliko wa seli macho na hivyo kusababisha saratani na kushindwa kuona kabisa.

Proffessor Li Li amesema dalili za mbadiliko wa seli macho mara nyingi hugundulika kwa watu wenye umri mkubwa (wazee), ila kwa sasa zinagunduliwa hata na kwa vijana wadogo hasa wenye umri wa kuanzia miaka 30-40 wanaongezeka kwa asilimia 3% na wote wakiwa ni watumiaji wa simu za mikononi (smartphone) kupitiliza.

Hata hivyo, kutumia simu (smartphone) gizani sio sababu ya tatizo la saratani ya macho tu pia inaweza sababishwa ugonjwa wa macho makavu, mtoto wa jicho na mwisho kupelekea kupoteza kuona.

Dalili za mwanzo za madhara yatokanayo na kutumia simu guzani ni kama vile vipele vidogo vidogo vinavyotibiwa kwa mionzi, sindano na madawa.

Madaktari bingwa wa macho 254 kutoka mahosipitalini pamoja na profesa Li Li wameshauri kuachana na tabia za kutumia simu gizani kwani husababisha matatizo ya maisha yako kwa ujumla.

Lakini pia inashauriwa utumie simu kukiwa na mwanga wa taa na sio gizani.

Nash Mc afunguka kuhusu wasanii kutojikubali
Antonio Nugaz awafariji mashabiki Yanga