Azam FC imemtangaza kocha wake wa zamani Aristica Cioaba kuwa kocha mkuu mpya akichukua nafasi ya Etienne Ndayiragije anayetarajia kutangazwa kuwa kocha wa kudumu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Azam imemtangaza Cioaba kupitia akaunti yake ya twitter mchana huu #WelcomeBackCioaba Azam FC tunayofuraha kubwa kuwafahamisha kuwa tumeingia mkataba wa mwaka mmoja na Kocha wetu wa zamani Aristica Cioaba.

“Cioaba anachukua mikoba ya Kocha, Etienne Ndayiragije, ambaye anatarajia kutangazwa kama Kocha wa kudumu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.”

Cioaba aliondoka Azam 2018, baada ya kushindwa kukubaliana na viongozi wa klabu hiyo kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya katika Ligi Kuu Bara.

Aidha, kama ilivyokuwa awali Cioaba, mwenye leseni ya juu ya ukocha ya UEFA Pro Licence, amerejea sambamba na Kocha wa viungo, Costel Birsan, aliyekuwa naye awali kipindi anaifundisha Azam FC.

Mara baada ya kuingia mkataba rasmi mapema leo Jumatatu, Cioaba ameishukuru Bodi ya Wakurugenzi na uongozi mzima wa Azam FC kwa kuendelea kuwa na imani naye.

“Naushukuru uongozi wa Azam FC kwa kuendelea kuwa na imani na mimi, kikubwa mimi sio mgeni hapa naijua timu, wachezaji wananijua na pia wanafahamu falsafa yangu, jambo kubwa ni kuendelea kuifanya timu kuwa juu pamoja na kushinda mataji,” alisema.

Baada ya kutimuliwa Cioaba nafasi yake ilichukuliwa na aliyekuwa kocha wa Singida United, Hans van Pluijm.

Ndayiragije anaenda timu ya Taifa, baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC kuridhia ombi la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wanaomuhitaji awe kocha mkuu wa kudumu baada ya kufanya vizuri akiwa na kikosi hicho akiwa kocha wa muda.

Azam FC tunamtakia kila la kheri, Ndayiragije katika majukumu yake mapya akiwa Taif Stars, ambapo tutakuwa naye sambamba pale atakapohitaji kutoka kwetu msaada kwenye masuala yake kiufundi.

 

Video: Mbosso athibitisha kunyimwa mtoto aliyezaa na Boss Martha, ''Akikua atanitafuta"
Bilioni 166.24 zakusanywa nchini Dar Kinara mapato ghafi