Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema hatojihisi furaha endapo ataondoka klabuni hapo bila kurejesha heshima ya kutwaa ubingwa wa soka nchini Engalnd.

Wenger amesisitiza jambo hilo, mbele ya vyombo vya habari huku akijua fika mkataba wake utafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Amesema anajua ana kazi nzito ya kurejesha heshima hiyo, lakini hana budi kuifanya kutokana na kiu ilinayowakabili mashabiki wa klabu ya Arsenal kwa zaidi miaka kumi sasa.

Mzee hyo kutoka nchini Ufaransa, amesema amekua akijaribu jambo hilo kufanikishwa kila mara, lakini changamoto kadhaa zimekua kikwazo kikubwa kwake.

Hata hivyo wenger hakuziweka wazi changamoto zinazomkwamisha kufikia lengo la kutwaa ubingwa wa nchini England zaidi ya kuendelea kubainisha harakati za kuhakikisha anairejeshea heshima Arsenal.

Kwa mara ya mwisho Arsenal ilitwaa ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini England katika msimu wa 2003-04, kwa kuweka rekodi ya kumaliza ligi hiyo bila kufungwa hata mchezo mmoja.

Kwa misimu miwiwli iliyopita ya 2013-14 na 2014-15, Arsenal iliwapoza machungu mashabiki wake baada ya kutwaa ubingwa wa kombe la FA, mara mbili mfululizo.

Brendan Rodgers Apata Kibarua Kingine
Magufuli: Namhurumia Dkt. Shein