Aliyekua meneja wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amebahatika kupata kazi, ikiwa ni majuma mawili tu yamepita tangu alipotimuliwa huko Anfield.

Rogders ambaye ni raia wa Ireland ya kaskazini, amepata kazi hiyo kimya kimya na hakutaka kuthibitisha kwa mtu yoyote wa karibu yake ama chombo cha habari.

Kilichoufahamisha umma juu ya Rodgers kupata kazi, ni ujumbe mfupu ulioandiokwa kwenye mtandao wa Twittwer na mtangazaji wa kituo cha televisheni na being Sports huko nchini Qatar, Richard Keys.

Keys ameandika, “Rodgers atakua nasi sambamba na Andy Gray mjini Doha na atafanya kazi ya kuchambua michezo ya ligi kuu ya soka nchini England”.

Mchambuzi mwingine ambaye anafanya kazi na kituo cha bein Sports, ambacho kina haki ya kuonyesha ligi ya nchini England, ni aliyekua kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Luis Javier García Sanz pamoja na aliyekua meneja wa klabu ya Cardiff City, Malky Mackay.

 

Soka La Zanzibar Laanza Kupata Nuru
Arsene Wenger Aahidi Neema Kabla Hajaondoka