Meneja wa Arsenal, Arsenal Wenger amewapongeza wachezaji wake kwa jinsi walivyopambana wakati wa mchezo ambao walitoka suluhu wakiwa ugenini dhidi ya Stoke City uliopigwa Jumatatu hii, kwenye uwanja wa Britannia.

Katika mchezo huo uliokuwa wa vuta nikuvute, licha ya Wenger kuonekana kufadhaishwa na timu yake dakika za mwisho, lakini anasema kuwa anawapongeza vijana wake waivyoweza kuzishitukia mbinu za Stoke City.

“Nadhani tulijaribu uwezo wetu wa kupambana, uwezo wetu wa upambana kwa pamoja na insi ya kujibu mashambulizi na tuliyajibu vizuri,” alisema Wenger.

Hata hivyo Mfaransa huyo pamoja na kuwapongeza wachezaji wake, alisema hakufurahi kutokana na kwamba hakuweza kufunga mabao.

“Lakini sina furaha kwa sababu nilitaka tufunge mabao lakini hatukufanya hivyo kwa leo,” alisema Mfaransa huyo.

 

Leicester City Inakaribia Kumnasa Amartey
Nemanja Vidic Atafuta Chaka La Kujificha