Polisi nchini Nigeria, inamtafuta mshukiwa wa ulaghai wa mtandaoni anayejulikana kama “yahoo boy”, aliyekimbia baada ya kumdunga kisu mfanyabiashara ya ngono hadi kufa na kuteketeza hoteli kando ya barabara ya Nnebisi huko Asaba, Jimbo la Delta.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na vyombo vya Habari nchini Nigeria, zimeeleza shuhuda wa tukio hilo alisema kuwa “Hatumjui mwanamume huyo, hatujui kilichotokea, lakini msichana amekufa sasat unahitaji polisi wasaidie kumkamata mtu huyo ili aweze kukabili sheria.” huku Afisa Uhusiano wa Polisi wa Jimbo, DSP. Bright Edafe, akithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Ikumbukwe kwamba, mapema mwezi Agosti, 2022 mfanyabiashara wa ngono alidungwa kisu na kunyongwa hadi kufa kwenye danguro maarufu huko Ughelli, ambapo yapo makao makuu ya Eneo la Serikali ya Mtaa ya Ughelli Kaskazini, katika Jimbo la Delta.
Marehemu huyo, aliyetambulika kwa jina moja la Confidence alikutwa amefariki chumbani kwake kwenye danguro baada ya kushindwa kujitokeza kuungana na wenzake kufanya kusaka wateja.