Jeshi la polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Askari wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) wa chuo Cha mafunzo ya Kijeshi Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kwa tuhuma za mauaji ya Lais Lemomo .
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapo amesema tukio hilo limetokea baada ya mwanajeshi kumpiga risasi Lemomo akiwa anachunga Mifugo.
Aidha Kamanda ACP Justine Masejo amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na upelelezi utakapokamilika taarifa kamili zitatolewa na sheria itafuata mkondo wake.
Naye Mkuu wa wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe na Mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli, Isack Joseph wamefika eneo la mauwaji hayo ambapo kumekuwa na mgogoro baina ya wafugaji na Jeshi.
Katika hatua nyingine ACP Kamanda Masejo, amesema jeshi la polisi linaendelea kumhoji mganga Mmoja wa kienyeji mkazi wa kata ya Sombetini kwa tuhuma za kumshawishi baba wa mtoto kufanya ukatilii dhidi ya mtoto wake.
Naye Mkuu wa wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe na Mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli, Isack Joseph wamefika eneo la mauwaji hayo ambapo kumekuwa na mgogoro baina ya wafugaji na Jeshi.