Mwalimu wa Shule ya Sekondari Momba, Shela Mwangoka amesimamishwa kazi na Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde kwa kudaiwa kumtusi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika kadamnasi ya watu kwa dhihaka kwa lugha zisizofaa kwa Rais.

Hayo yamebainika baada ya mkutano wa shina kati ya wananchi wa Kijiji cha Washo Kata ya Myunga Wilaya ya Momba Emily Skanyika na Jacob Miyala ambao walitoa kero yao kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa CCM Shaka Hamdu Shaka kuwa mwalimu huyo amekua akitoa lugha za matusi mara kwa mara hali ambayo inawachafua wananchi hao kuona Rais wao anatukanwa.

Kwa upande wake Naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde amesema amefanya uchunguzi mdogo baada ya kusikia malalamiko hayo kujiridhisha na kugundua kua ni tabia ya Mwalimu huyo kufanya hivyo na mara ya mwisho ni wiki moja iliyopita akiwa sokoni alipoona Rais Samia kaongeza madaraja na mishahara kwa watumishi wa umma akasema ni hongo ili amuunge mkono akasema hawezi muunga mkono sababu ni mwanamke.

Ahadi zamiminika Raja Casablanca
Bilioni 42 kuboresha kituo cha kupozea umeme Tabora