Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 42 kuboresha kituo cha kupozea na kusambaza umeme cha Kiloleni, wilaya ya Tabora mjini, mkoani Tabora ili kuimarisha huduma ya umeme.

Akizungumza alipotembelea kituo hicho Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato amesema kuwa, Tabora ni Mkoa wa kimkati wenye fursa nyingi za maendeleo ikiwemo migodi, kilimo na viwanda hivyo, unahitaji kuwa na umeme wa uhakika kuwezesha shughuli za kiuchumi kufanyika kwa kasi.

Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato akizungumza na Waandishi wa Habari alipotembelea  kituo cha kupozea na kusambaza umeme cha Kiloleni kilichopo Tabora mjini, mkoani Tabora

Ameongeza kuwa, umeme wa uhakika mkoani Tabora utawezesha uendeshaji wa train ya kisasa (Standard Gauge) ambayo uzinduzi wa shughuli za ujenzi wake unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Aidha, Naibu Waziri Byabato amebainisha kuwa, Kituo cha kupozea na kusambaza umeme cha Kiloleni ni miongoni mwa vituo 9 vinavyotarajiwa kuboreshwa mkoani Tabora ili kuwa na umeme wa uhakika.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa Kituo cha Kiloleni Frank Chengula namna chombo cha kuongozea mitambo kinavyofanya kazi kituoni hapo

Sambasamba na hayo Naibu Waziri Byabato, ameagiza kutengenezwa kwa transfoma iliyoharibika  ndani ya Mwezi Julai, 2021 ili kuongeza nguvu ya umeme kituoni  Kiloleni licha ya kuwa kuna transfoma moja inayofanya kazi.

Asimamishwa kazi kwa kumtusi Rais
Kassim Majaliwa atoa siku 7 kwa kamati ya uchunguzi kariakoo