Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano a Tanzania Kassim Majaliwa ametoa siku saba kwa kwa timu iliyoundwa kuchunguza chanzo cha ajali ya moto katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Ametoa agizo hilo Leo Julai 11, 2021 wakati akizungumza na wahanga wa moto huo, na kusema timu hiyo itatoa pia ushauri wa kitaalamu, amesema kuwa endapo itabainika kuna hujuma zozote zimefanyika serikali haitasita kuchukua hatua stahiki.

“Ndugu wafanyabiashara, nimekuja kuleta salam za pole kutoka kwa Rais Samia Suluhu, Kuja kwangu leo asubuhi ilikuwa ni moja ya maelekezo yake bna kuja kuona hali halisi ya kuungua kwa bidhaa mbalimbali ambazo ndizo zilizokuwa zinaipa hadhi ya eneo hili la Kariakoo”

Moto huo ambao umeteketeza maduka ya wafanyabiashara katika soko hilo ulinza kuwaka majira ya saa mbili usiku Julai 10, 2021.

“Nimeona hali halisi na kwa namna ninavyojua soko la Kariakoo, hasara kubwa inatarajiwa kupatikana, kama ambavyo nimetangulia kuwapa pole, nirudie tena kuwapa pole kwa kupoteza mali, fedha lakini pia hata muelekeo wa kufanya shughuli zenu za kibiashara hapo baadae,” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Aidha vyombo vya ulinzii na usalama vimeendelea kusalia katika eneo la tukio ili kuhakikisha huo hauendelei.

“Eneo hilo kwa sasa ni hatarishi kwasababu bado moto unafuka mwingi, hatujajua bado kuna maeneo yana milipuko kama vile mitungi ya gesi ambao wanatumia gesi lakini kuna nyaya nyingi sana za umeme, kuna mitambo mingi iliyokuwa inauzwa lakini pia ilikuwa inatumika ndio maana eneo hili sio salama,” Amesema Waziri Majaliwa.

Aidha amewasihi wafanyabiashara wote kuwa watulivu, kwani Serikali inalifuatilia suala hilo kwa makini ili kujua nini chanzo cha moto huo.

Kamati ya uchungu iliyoundwa itahusisha sekta mbalimbali ikiwemo :-

  1. Ofisi ya RAS
  2. Ofisi ya Rais Ikulu na TAMISEMI
  3. Ofisi ya waziri mkuu-Mkurugenzi wa Maafa
  4. Vyombo vya ulinzi na usalama vinne(JWTZ, Polisi)
  5. TBA(Mhandisi wa majengo na Mhandisi wa umeme kwenye majengo)
  6. TANESCO
  7. Mwanasheria Mkuu
  8. Mkurugenzi wa Mashtaka

Moto huo ambao umeteketeza maduka ya wafanyabiashara katika soko hilo ulinza kuwaka majira ya saa mbili usiku Julai 10, 2021.

Bilioni 42 kuboresha kituo cha kupozea umeme Tabora
Naibu Waziri Kasekenya ziarani ukaguzi wa miundombinu