Askari wawili wa wanyama pori, wameuawa na mwingine kujeruhiwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo katika Mbuga ya Kitaifa ya Virunga, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.
Taasisi ya Uhifadhi wa Mazingira nchini Kongo (ICCN), imesema walinzi hao walikuwa wakishika doria katika eneo kuu la mbuga hiyo, na waliposhambuliwa kabla ya kufariki huku wenzao wakiwashuku washambuliaji wa kundi la Maimai.
Virunga, ndiyo eneo kubwa kwenye mpaka wa Uganda na Rwanda, ikiwa ni hifadhi kongwe zaidi barani Afrika na ikijulikana ulimwenguni kote kama hifadhi ya wanyama adimu, wakiwemo sokwe wa milimani.
Hifadhi hiyo, pia hutumika kama maficho ya vikundi vyenye silaha vinavyofanya kazi katika eneo hilo kwa miaka mingi.