Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amesema kuwa mwalimu wa shule ya msingi kutoka mkoani humo, atakayeongoza kwa ufaulu wa alama A atajipatia zawadi ya shilingi laki 5 za kitanzania.
“Mwalimu atakayeongoza kwa ufaulu wa alama A nyingi kimkoa katika mitihani ya darasa la saba atapewa shilingi laki 5 (masomo ni 5 na kwa kila somo ni shilngi laki 5)” amesema Mtaka.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa Shule itakayoingia 10 Bora Kitaifa watapewa shilingi Milioni 3 za kitanzania kama zawadi ya shule iliyowakilisha mkoa huo vizuri katika mtihani wa taifa kwa darasa la saba.
Sambamba na zawadi kwa walimu na shule zitakazofanya vizuri ,uongozi wa mkoa utawapeleka ziara ya utalii kwenye hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikiwa kama shukrani na pongezi kwa matokeo mazuri.
“Wilaya itakayoingia 10 Bora kitaifa Walimu wake wote wataenda ziara ya Utalii Hifadhi yetu ya Serengeti,”.
Mwaka uliopita uongozi wa mkoa huo ulitoa zawadi ya shilingi Laki 3 kwa watoto wanne waliongia 10 bora kitaifa kutoka shule za serikali.