Madaktari nchini India wamefanya upasuaji wa kipekee na kuondoa uvimbe wa wa kilo 1.8 kutoka kwa mwanamume mwenye umri wa miaka 31.

Madaktari hao wamesema kuwa uvimbe huo huenda ukawa ni mkubwa zaidi kuwahi kutolewa kwenye ubongo wa binadamu.

Upasuaji huo, ambao ulifanyika kwa muda wa saa saba, tarehe 14 Februari katika hospitali ya Nair mjini Mumbai magharibi mwa nchi hiyo, lakini taarifa za upasuaji huo hazikutangazwa moja kwa moja kwa sababu madaktari hawakuwa na uhakika kama kweli walifanikiwa.

“Sasa ni suala tu lake kupona, lakini maisha yake hayamo hatarini tena na hatukuweza kutanga moja kwa moja kwasababu hatukuwa na uhakika kama tumefanikiwa,” amesema Dkt Trimurti Nadkarni, mkuu wa upasuaji.

Aidha, Santlal Pal kutoka jimbo la Uttar Pradesh kaskazini mwa India, amekuwa akiishi na uvimbe huo kwa muda wa miaka mitatu.

Hata hivyo, Madaktari wamesema kuwa Pal alipoteza uwezo wake wa kuona kutokana na uvimbe huo ambao amedumu nao kwa muda mrefu.

Wanafunzi wengine wa kike watekwa na Boko Haram wakiwa shule
Video: Msajili aitisha Chadema, Simanzi tupu kuagwa Akwilina