Baada ya miaka miwili ya ukimya katika muziki, mkali wa āMuhogo Andaziā, Nuru The Light amerejea na wimbo mpya alioupa jina la āLā.
Nuru ambaye muda mwingi alikuwa nchini Sweden, wiki iliyopita aliachia huo ambao umetayarishwa kwa kiwango kizuri cha muziki wa āLiveā katika studio za Joevibes Production, zilizoko nchini Sweden.
Akiongea na Dar 24, Nuru amesema kuwa āLā katika wimbo huo wa mapenzi ina maana nyingi kubwa na chanya ambazo heruhi hiyo inaziwakilisha.
āāLā ina simamia vitu vingi positive, inaweza kuwa Love, Lough, Life na nyingine,ā alisema. āJina la wimbo huu linatokana na ubunifu na kuonesha kuwa hata herufi moja tu inaweza kusimamia wimbo mkubwa kama huu na ukafanya vizuri,ā aliongeza.
Nuru ambaye aliwahi kufanya vizuri na nyimbo kama Muhogo Andazi, Walimwengu, Msela na Nsubiri Usilale amekamilisha video ya āLā aliyofanya na muongozaji mkongwe, Adam Juma na hivi karibuni atarajia kuizindua kwa njia ya kipekee.
āNashukuru Adam Juma hajawahi kuniangusha katika video zote, hii video ya āLā ni nzuri sana na naamini mashabiki wangu wataipenda kwa moyo wote. Nakamilisha mipango ya uzinduzi wa video, utakuwa wa kipekee, baada ya hapo mtaiona kwenye TV na mitandaoni,ā alisema.
Mwimbaji huyo wa kike ambaye ameishi Sweden kwa muda mrefu na hivi sasa yuko nchini kwa ajili ya kusimamia projects zake kadhaa, amewaahidi mashabiki wake kuwa ingawa yuko ughaibuni, hatawaangusha na ataendelea kufanya muziki mzuri kwa ajili ya nyumbani Tanzania.
Hii ni video ya wimbo wa Nsubiri Usilale, moja kati ya kazi alizofanya na Adam Juma.
Sikiliza hapa wimbo mpya wa Nuru The Light, āLā: