Shabiki wa klabu ya Simba SC alietembea kwa miguu kutoka Kigoma amewasili salama jijini Dar es salaam.
Michael Filbert alijitoa muhanga wa kutembea kutoka Kigoma kuelekea Dar es salaam, kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa watani wa jadi utakaopigwa Julai 3, Uwanja wa Mkapa.
Kwa mujibu wa taarifa zilitolewa na klabu ya Simba kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo, shabiki huyo ametumia siku 15 katika safari yake.
Michael amepokewa na kundi la Simba Ushirikiano kutoka Kigogo.
Kwa kuonesha Uongozi wa Simba upo pamoja na shabiki huyo, Kaimu Mkurugenzi wa Wanachama, Hamisi tawi la Simba Ushirikiano Kigogo katika mapokezi ya shabiki Michael.
Simba SC inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 70, kesho Jumanne itacheza dhidi ya Mbeya City, kisha itakwenda mjini Songea mkoani Ruvuma kucheza mchezo wa Kombe la Shirikishi ASFC dhidi ya Azam FC, mwiahoni mwa juma hili.
Baada ya mchezo huo itarejea jijini Dar es salaam kjkipiga dhidi ya mtani wake Young Africans Julai 03.