Benchi la Ufundi la Klabu ya Azam FC limeahidi kufanya usajili wa kishindo kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ‘NBCPL’, Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ na Kombe la Shirikisho Barani Afrika ‘CAFCC’.

Kocha wa timu hiyo, Kally Ongala amesema licha ya kukosa taji lolote msimu huu hawajakata tamaa na wanakwenda kujipanga upya.

“Tutakwenda kukiboresha kikosi chetu msimu ujao kwa kusajili wachezaji ambao wataleta ushindani na si ukubwa wa majina,” amesema Ongala

Kocha huyo amesema msimu uliopita ulikuwa mgumu na wenye upinzani mkubwa na kuahidi kurekebisha mapungufu yote yaliyojitokeza msimu huu.

Amesema watarudi kivingine msimu ujao na kuomba mashabiki wao waendelee kuwaunga mkono ili watimize malengo yao. “Tunaomba mashabiki wetu wasikatishwe tamaa na matokeo tuliyoyapata msimu huu bali waendeleze ushirikiano msimu ujao, kwani kila kitu kitakaa sawa.” amesema

Rais Samia atembelea ujenzi Hotel ya kitalii nyota tano
RFEF, CBF kupinga ubaguzi wa rangi