Baada ya kuwashtua wadau wa soka la Bongo kwa kufanya usajili wa beki wa kushoto Edward Charles Manyama, Uongozi wa Azam FC umefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu umafia walioufanya.
Kabla ya kubainika amesaini Azam FC, Manyama alitajwa kujiunga na mabingwa wa tanzia Bara Simba SC siku mbili zilizopit, lakini maamuzi alioyachukua yamethibitisha tarifa hizo hazikua za kweli.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Thabit Zakaria (Zaka Zakazi) amesema wamekamilisha usajili wa beki huyo, kwa kuzingatia taratibu zote, na siku zote Azam FC wamekua wakifanya mambo yao kwa kuzingatia kanuni na sheria.
Amesema walikua wanahitaji huduma ya beki huyo ambaye anamalizia mkataba wake ndani ya Ruvu Shooting, na waliamua kukaa kimya kwa kuzipuuza tarifa ambazo ziliibuka kumuhusu Manyama kujiunga Simba SC.
“Sisi Azam FC huwa hatusajili kwa tetesi hasa kwa sasa, sisi ni vitendo tu. Kuhusu sijui alikuwa kasajiliwa na Simba mi sijui”
“Sisi tulienda kwenye klabu yake (Ruvu Shooting) tukaongea na klabu yake kwa sababu bado hajamaliza mkataba, klabu ikaturuhusu tukamsajili” amesema Zaka Zakazi,Afisa Habari wa Azam FC.
Manyama alijiunga na Ruvu Shooting wakati wa Dirisha dogo la usajili mwishoni mwa mwaka jana, akitokea Namungo FC.