Wakati taarifa zikieleza kuwa klabu ya Young Africans imekamilisha dili la kumsajili beki wa pembeni na nahodha wa AS Vita Djuma Shaban, Mkuu wa Idaya ya Habari na Mwasilino ya klabu hiyo Hassan Bumbuli amaempiga kijembe Haji Manara.

Huenda Bumbuli amefanya hivyo kwa kujiamini kufuatia taarifa za kukamilika kwa dili la Djuma kutua Young Africans kama inavyoelezwa huko jijini Kinshasa, DR Congo.

Bumbuli amesema “Ukisema huyu mchezaji ghali sana, jua umejisemea wewe na klabu yako iliyozoea MIDONDO, acha kujipa mamlaka ya kuwasemea wengine Utaaibika, ona sasa Jamaa ni Young Africans, sema mwingine nani ghali sana tukamng’oe. Kwetu ukisema “Ghali” tunaongeza “b”  

Haji Manara jana aliandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii,  akigusia gharama kubwa ya usajili wa Djuma.

Manara aliandika: Djuma Shabani thamani yake ni Dola laki tano hapo weka kando mshahara.

Nasikia ndugu yangu Ghalib keshajibiwa bei yake , na mm najuwa TP Mazembe na Ahly pamoja na Mamelodi washatuma ndoano kwake

Sasa nataka nione kama yupo serious na utopolo yake, au ndio yale yale ya kina Sarpong ?

Tungependa tuone msimu ujao ligi yetu inazidi kuwa na Quality players like him.

Sasa Shekh GSM toa mzigo ili tukiwa tunakufunga tufunge Uto iliyo na nafuu kidogo.

Azam FC: Tunamaliza kimya kimya
Wakala wa Bwalya aichimba mkwara Simba SC