Wakala wa mchezaji Walter Bwalya, amesema mchzaji wake huenda akaondoka kwa mabingwa wa soka Barani Afrika Al Ahly mwishoni mwa msimu huu.

Paricha Chikoye wakala wa mshambuliaji huyo kutoka DR Congo amekaririwa na tovuti ya Goal akithibitisha taarifa hizo.

Amesema mchezaji wake amekua na changamoto ya kushindwa kufikia malengo ya Al Ahly ambayo ilimsajili mwanzoni mwa msimu huu.

Hata hivyo ameutaka uongozi wa Simba SC kuacha kuvumisha taarifa za kuwa mbioni kumsajili Bwalya kupitia mitandao ya kijamii.

Amesema klabu hiyo ya Tanzania kama inamuhitaji mchezaji wake inajua njianza kufuata, lakini akasisitiza kuwa mabingwa wa Tanzania huenda wakakwama kutikana na fedha kubwa ya usajili ambayo itamuingiza sokoni Bwalya.

“Ipo wazi kwamba Al Ahly wanataka kumuuza mteja wangu kutokana na kuona kwamba haendani na mfumo ya timu yao hivyo hamna namna lazima wamuuze.

“Imekuwa tetesi kwamba anahitajika na Simba SC ila ukweli ni kwamba mabingwa hao wa Tanzania hawana uwezo wa kumlipa fedha ambazo tunahitaji kutokana na mkataba wetu na Al Ahly.

“Kumpata Bwalya sio jambo jepesi na sisi tunahitaji fedha kubwa na siwezi kukutajia kwa sasa hivyo tusibiri na tuone.” Amesema Chikoye

Bumbuli amchimba Haji Manara
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Ngrebada, ajiuzulu