Kiongozi wa juu nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei ameonekana kuzidiwa na huzini na kuamua kuondoka baada ya kuongoza ibada ya sala ya kuaga miili ya aliyekuwa Rais wa taifa hilo Ebrahim Raisi na maafisa wengine waliokufa kwenye ajali ya helikopta, zoezi lililoshuhudiwa na maafisa wa ngazi za juu zaidi ya 40 kutoka mataifa ya kigeni mjini Tehran.

Khamenei ameongoza shughuli hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Tehran, ambapo vilio vilisikika kutoka kwa waombolezaji waliokusanyika kwa ajili ya kuwaaga viongozi wao, wakati majeneza yao yaliyokuwa yamezungushiwa bendera ya Iran, yalipopangwa mbele ya maafisa wandamizi.

Khamenei aliongozwa ibada hiyo akitumia kitabu kitakatifu cha Kiislamu cha Quran na aliondoka mara baada ya sala ambapo wakati wote Rais wa mpito wa Iran, Mohammad Mokhber alikuwa amesimama karibu na Khamenei akionekana kububujikwa na machozi.

Miongoni mwa waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Maafisa waandamizi wa Kikosi cha Walinzi wa Kimapinduzi, chenye ushawishi mkubwa nchini humo, akiwemo Kiongozi wa Wanamgambo wa Hamas wa Palestina, Ismail Haniyeh.

MAKALA: Bodaboda ni asali inayokupa shubiri
Dkt. Kijaji: Mauzo ya bidhaa soko la Ulaya yameongezeka