Wanawake na Vijana nchiji, wametakiwa kujitokeza kushiriki katika kongamano la Biashara linalotarajiwa kufanyika Mei 28 hadi 31, 2024.

Hayo yamebainishwa jijiji Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa Taasisi ya Wanawake Wafanyabiashara Kimataifa, Noreen Mawalla wakati akizungumzia kuhusu maadhimisho ya siku ya Afrika yatakayojumuisha kongamano na maonesho ya biashara ya kimataifa.

Amesema, kongamano hilo ambalo ni la tatu litahusisha wajasiriamali, wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa serikali na wadau wa maendeleo wakilenga kujenga uelewa wa pamoja juu ya manufaa ya kufanya biashara katika eneo la soko huru la Afrika.

 

“Kama mnavyofahamu Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimerudhia katika eneo la soko huru la Afrika, na ziko takeibani nchi 54 lengo lake ni kuwa na soko la pamoja katika Bara Zima la Afrika, kwa mara ya tatu tunaandaa kongamano hili kutoa elimu na watu kujua fursa zinazopatikana katika eneo la soko huru la Afrika,” amesema.

Naye Mratibu wa kongamano hilo ,Meshack Robert amesema kongamano hilo linashirikisha mataifa ya afrika hivyo ni fursa kwa vijana Wanawake kutangaza na kuuza bidhaa zao.

Amesema, bidhaa nyingi zinazotumika kwenye mataifa mbalimbali zinatokea Afrika, hivyo uzalishaji unatakiwa kuwa mkubwa utakaowezesha bidhaa kukuzwa maeneo mbalimbali na kukuza uchumi.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 23, 2024
MAKALA: Bodaboda ni asali inayokupa shubiri