Kikosi cha Azam FC kimeanza safari ya kurejea jijini Dar es salaam, baada ya kuichabanga Mbeya City FC bao 1-0 katika mchezo wa Mzunguuko wanne wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jana Jumanne (Septemba 13), katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokione.
Azam FC ilipata ushindi huo kupitia kwa Mshambuliaji wao kutoka DR Congo Idris Ilunga Mbombo katika dakika ya 61.
Azam FC kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii imethibitisha taarifa za kuondoka kwa kikosi chao jijini Mbeya kurejea Dar es salaam.
Taarifa hiyo imeandikwa: “Baada ya kuichapa Mbeya City, kikosi chetu kimeanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam asubuhi hii.”
weareazamfc #timuborabidhaabora
Ushindi wa Azam FC dhidi ya Mbeya City umeifanya klabu hiyo ya Chamazi-Dar es salaam kufikisha alama nane zinazoiweka kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Azam FC imezifunga Kagera Sugar na Mbeya City FC na kutoka sare michezo miwili dhidi ya Geita Gold FC na Young Africans.