Kampuni ya Azam TV Media Limited imeshinda tenda ya kuonyesha michezo Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mkataba wa Shilingi Bilioni 225.6, ambao utadumu kwa miaka miaka 10,
Kwa mara ya kwanza TFF na Azam TV Media Limited waliingia mkataba wa kuonyesha michezo Ligi hiyo Mnamo Mwaka 2012 na baada ya mkataba huo kumalizika mwaka 2006, TFF ili tangaza tenda kwa Media mbali mbali ambazo zinataka kuonyesha ligi hiyo na Azam Media imeibuka Mshindi.
Mkataba wa pili kati ya TFF na Azam Media Limited ulikuw ana thamani ya Shilingi bilioni 23.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari pamoja na viongozi waalikwa waliokuwa katika hafla hiyo ya kutia saini mkataba wa Haki za Television, katika Hotel ya Hyat iliyo Posta jijini Dar es salaam, Rais wa TFF, Wallace Karia amesema: “Nachukua fursa hii kuwapongeza Azam Media Limetide chini ya Mkurugenzi wao Tido Muhando kwa kufanikiwa kushinda tena zabuni hii hivyo kufanya kazi na TFF pamoja na Bodi ya Ligi Tanzania, chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kuendesha ligi hii,”
Hata hivyo TFF Imesema kuwa kwa msimu huu kutakuwa na haki za matangazo ya redio pomoja na Online TV ambapo mchakato wake umeshatangazwa kwa Vyombo vitakavyotaka kuruka Mubashara Upande huo.