Baada ya jana kufanikiwa kuiandikishia ushindi wa kwanza klabu yake ya Yanga, mshambuliaji mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutokea Mgambo JKT ya Tanga, Malimi Busungu amejigamba na kueleza nia yake ya kuwa juu ya wapachika mabao.

Busungu ambaye aliifungia magoli mawili timu yake iliyoibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Telecom, amesema nia yake ni kuwafunika washambuliaji wote na kuibuka mfungaji bora hivyo kwake kazi ndio kwanza inaanza.

“Niameanza vizuri Yanga kwenye mashindano haya ya kimataifa, namshukuru Mungu kwa kunijalia kuweza kufunga magoli mawili kwa kushirikiana na wachezaji wenzagu”, alisema busungu baada ya mchezo kumkalizika.

“Hii ni mechi yangu ya kwanza kwenye Kagame lakini nimefanikiwa kufunga magoli mawili, wafungaji wanaoongoza wanamagoli matatu kama ntaendelea kupata nafasi ya kucheza naweza kuibuka mfungaji bora maana hatuwezi kujua mpaka sasa nani atakuwa mfungaji bora na atafunga magoli mangapi”, aliongeza.

“Nataka kuendelea kufunga zaidi pale ntakapopata nafasi, mashabiki waendelee kutupa sapoti naamini tutafanya vizuri sana. Tulianza mchezo tukiwa na presha kubwa ya kutaka kufunga magoli mengi kipindi cha kwanza lakini matokeo yake tukapoteza nafasi nyingi kwasababu ya papara, lakini tulipoenda mapumziko makocha wakatuambia tutulie, tulivyorudi tukafanikiwa kufunga magoli mengine mawili”, alifafanua.

Mbali na kupachika magoli mawili, muda mwingi mshambuliaji huyo alikuwa akiisumbua safu ya ulinzi ya Telecom. Mara baada ya mchezo huo kumalizika, Busungu alitangazwa kuwa mchezi bora wa mchezo huo (man of the match) na kukabidhiwa king’amuzi cha DSTV na kituo cha television cha Super sport.

Messi Alimtesa ‘Kweli’ Rais Wa Gabon
CCM: Tume Ya Uchaguzi Imetudhalilisha