Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika katika makosa mbalimbali ya uhalifu.
Jeshi hilo linamshikilia Anthony Costantine Maningu (50), kwa kumpiga kichwani na kitu kizito na kumsababishia kifo mtoto wake aitwaye Veronica Anthony (17), mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Kayenze, wilaya ya Ilemela mkoani humo.
Mzazi wa binti huyo, amesema kwamba tukio hilo lilitokea baada ya kile anachokidai kuwa Veronica kurudi nyumbani kwao akiwa amechelewa majira ya usiku kitendo kinachodaiwa kumkasirisha baba yake mzazi na kuamua kuchukua uamuzi huo.
Kamanda Muliro amesema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya bugando kwa uchunguzi wa daktari na mtuhumiwa ambaye ni baba mzazi wa marehemu amekamatwa na atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.
Katika hatua nyingine, jeshi hilo linamshikilia Mussa Gabriel Majuto (35), mkazi wa Mwanza kwa kumpiga na kitu kizito utosini na kumuua Emmanuel Joseph, miaka (49), kwa kile kinachodaiwa kuwa marehemu alikuwa akimtuhumu mtuhumiwa kumwibia simu yake aina ya Tecno ya batani yenye thamani ya tsh 40,000/=.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya mkoa ya sekou toure kwa uchunguzi wa daktari, na mtuhumiwa amekamatwa, upelelezi unakamiliswa na atafikishwa mahakani haraka iwezekanavyo.