Baba mzazi wa Kiungo Mshambuliaji wa Taifa Stars, Happy God Msuva amesema dili la mwanae Simon Msuva si tu haliwezekani Young Africans bali kwa klabu yoyote ya Tanzania.
Mzazi huyo ambaye ni msimamizi wa staa huyo wa zamani wa Young Africans, amekiri kusikia mwanae akihusishwa na Young Africans lakini anachojua kwa sasa akili yake haipo Tanzania.
Inafahamika kuwa Young Africans wanasaka saini ya mmoja kati ya Msuva, Mkongomani Macabi Lilepo na George Mpole wa FC Lupopo.
Amesema habari zinazoendelea bado haziendani na malengo makubwa ya mwanae kuendelea kukipiga nje ya nchi na muda wowote kuanza sasa dili likitiki na ataondoka nchini.
“Mwanangu ananiambia, baba bado nataka kucheza nje ikitokea kucheza hapa nyumbani labda baadae lakini kwa sasa acha nikapambane huko kwanza,” amesema Baba mchezaji huyo
“Mambo yakikamilika tutaweka wazi lakini wanamichezo wajue sasa hivi Msuva kucheza hapa nyumbani hapana acha akapambane kama ambavyo anahitaji yeye,” amesema huku Simba SC nao wakidai kuzungumza na mchezaji huyo juma hili ingawa hawakufikia mwafaka wowote.
Sio mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kuhusishwa na Young Africans, lakini wameongeza nguvu kutokana na uhitaji uliopo kwenye safu ya ushambuliaji hasa baada ya kuondoka kwa Fiston Mayele.
Kwa mujibu wa TFF Young Africans inaweza kumuingiza Msuva kwenye usajili wao wa CAF kwa faini, lakini ni kama utetezi wao utakubalika.