Kocha Mkuu wa Kagera Sugar FrancisBaraza leo Alhamis (April 08) anaanza mtihani wa kupambania alama tatu za Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na klabu mpya, baada ya kuachana na Biashara United Mara ya mkoani Mara.
Kagera Sugar leo itakua ugenini ikicheza dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokione jijini Mbeya, ukiwa ni mchezo wa mzunguuko wa 25 wa Ligi Kuu, ambayo ilisimama kupisha maandalizi ya Taifa Stars na msiba wa aliyekua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Joseph Magufuli.
Kocha Baraza amesema anatambua mtihani wa kuiendesha klabu yake mpya kwenye mchezo huo utakua mgumu, lakini hana budi kutumia mbinu alizowafundisha wachezaji wake, ili kupata alama tatu muhimu ambazo zitakua za kwanza kwake tangu alipokabidhiwa mikoba ya Kocha mzawa Meck Mexime.
“Wacha nikwambie, sitacheza kwa kuhofia, nafasi tuliyopo kwenye msimamo haitufanyi kucheza kwa kuzuia, nitajitahidi kuwahimiza vijana wangu wacheze kwa kushambulia zaidi Ili kuweza kushinda mchezo huu.” Amesema kocha huyo kutoka nchini Kenya.
Kagera Sugar ipo ugenini huku ikiwa imeshajikusanyia alama 25 zinazowaweka kwenye nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Mbeya City ikiwa kwenye nafasi ya 16, ikiwa na alama 20.
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguuko wa 25 utakaochezwa leo Alhamis (April 08), utakua kati ya Namungo FC ambao watakua nyumbani Uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa mkoani Lindi wakicheza dhidi ya Ihefu FC waliofunga safari kutoka mkoani Mbeya.
Michezo mingine ya mzunguuko wa 25 itakayochezwa mwishoni mwa juma hili.
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa.