Sakata la kuvushwa kinyemela kwa maelfu ya makontena  Bandarini yaliyoisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 48 limeendelea kuchukua sura mpya baada ya kubainika kuwa taasisi za dini ni miongoni mwa watuhumiwa.

Hayo yamebainika kupitia orodha mpya iliyotangazwa jana na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) yenye majina ya kampuni 283 ambayo ina nyongeza ya taasisi/makampuni mengine 40 ambayo hayakutajwa kwenye orodha ya awali.

Orodha hiyo iliyosainiwa Desemba 24 mwaka huu, imeyataja pia mashirika ya dini ambayo ni Baraza la Kikristo Tanzania (CCT),  Shirika la misaada la Kanisa Katoliki pamoja na Caritas Tanzania.

Tangazo hilo limezitaka taasisi zote zilizotajwa kwenye orodha hiyo kuchukua barua zao TPA kwa ajili ya kufanya uhakiki wa malipo ya ushuru.

 

Baby Madaha aanguka Chooni
Wanaoumaliza Mwaka na Baraka za Uteuzi wa Magufuli Hawa Hapa