Msanii wa Bongo Flava ambaye ni muigizaji wa Filamu za kiswahili (Bongo Movies), Baby Madaha ameripotiwa kupata ajali baada ya kuanguka akiwa maliwatoni, ajali iliyompelekea kuvunjika mguu wake wa kulia.

Kwa mujibu wa msanii huyo, ajali hiyo ilimkuta majira ya saa kumi alfajiri alipokuwa ametoka katika starehe. Alisema kuwa baada ya kuanguka katika chumba hicho cha faragha, alijisikia maumivu makali ya mguu ambayo hakuwahi kuyasikia kabla.

“Sijawahi kupata maumivu makali kama haya maana baada ya kudondoka chini nilijisikia sina nguvu wala sikuweza kusimama, nikalazimika kuukanyagia mguu wangu,” Baby Madaha alieleza.

Baby Madawa akiwa nyumbani kwake siku chache baada ya kupata ajali

Baby Madaha akiwa nyumbani kwake siku chache baada ya kupata ajali

Alisema kuwa asubuhi alilazimika kufika katika hospitali ya AAR iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam na baada ya kufanyiwa vipimo alibainika kuwa alikuwa amevunjika mguu. Alipata matibabu na hadi sasa amefungwa P.O.P (Muhogo). Hadi sasa anaendelea kuuguza mguu wake.

Chanzo cha ajali hiyo ni ulevi wa pombe uliomzidia usiku huo.

Chanzo: Global publishers

 

Kamanda Kova Aliaga Jeshi la Polisi, Kustaafu rasmi leo
Baraza la Kikristo, Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki Yatajwa Sakata la Makontena

Comments

comments