Klabu ya Barcelona imesema mashabiki wake hawatoweza kupata tiketi za kuingia katika mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid utakaopigwa katika uwanja wa Wanda Metropolitano Octoba 14 mwaka huu kutokana na matatizo ya vifaa katika uwanja huo.

Hii itakuwa ni mara ya pili mfurulizo kwa Barcelona kucheza bila mashabiki wake kufuatia Jumapili iliyopita kucheza bila mashabiki katika uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp katika mchezo wao dhidi ya klabu ya Las Palmas kutokana na sababu za kisiasa za jimbo la Catalonia.

Barcelona wametangaza katika tovuti yao kuwa Atletico Madrid hawatoweza kutoa tiketi zilizotakiwa kutolewa  kwa mashabiki wa Barcelona.

Kumekuwa na mvutano wa kisiasa katika jimbo la Catalonia huku jimbo hilo likitaka kujitenga na Hispania jambo litakalosababisha klabu ya Barcelona inayotoka katika jimbo hilo kuwa njia panda.

Haijulikani iwapo jimbo la Cataonia litajitenga na Hispania klabu ya Barcelona itacheza katika La Liga au itacheza katika ligi ya nchi nyingine.

 

 

 

Vanessa ‘ateka’ tuzo za kimataifa, fanya haya umpe ushindi
Nassari asubiri ushahidi mwingine kutoka Arusha