Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha, amechimba mkwara mzito akisema kwamba, ametua ndani ya klabu hiyo kwa sababu moja kubwa ambayo ni kuendeleza rekodi yake ya kushinda makombe.
Benchikha ambaye ametua Simba SC kuchukua mikoba ya kocha kutoka Brazil, Roberto Oliveira, ana kazi kubwa ya kuhakikisha Simba SC inarudisha makombe ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Tanzania Bara ‘ASFC’ ambayo yamebebwa na Young Africans kwa misimu miwili mfululizo sasa.
Kocha huyo ametua Simba SC akiwa na wataalamu wengine wa Benchi la Ufundi ambao ni kocha msaidizi, Farid Zemit na Kocha wa Viungo, Kamal Boudjenane, huku akiwa na rekodi ya kushinda zaidi ya mataji 15 akiwa na timu mbalimbali.
Benchikha amesema: “Nimefurahi kujiunga na timu hii, kila mmoja anajua Simba SC ni miongoni mwa timu kubwa Afrika kwa sasa na nimevutiwa na mipango yao.
“Niko hapa kwa ajili ya kushinda na kuendeleza rekodi yangu ya mafanikio ikiewemo kushinda makombe, nafahamu hilo ndilo lengo kubwa la timu hii hivyo jambo pekee nalohitaji ni ushirikiano.