Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Henry Kissinger amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100 nyumbani kwake Connecticut, alitekeleza jukumu muhimu la kuleta mgawanyiko katika sera za kigeni za Marekani wakati wa Vita Baridi, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.

Kissinger alihudumu kama Mwanadiplomasia mkuu wa Amerika na mshauri wa usalama wa kitaifa wakati wa tawala za Nixon na Ford, licha ya kuondoka madarakani katikati ya miaka ya 1970, aliendelea kushauri vizazi vya viongozi kwa miongo kadhaa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kutoka kwa Kissinger Associates, kampuni ya sera aliyoanzisha, haikutoa sababu ya kifo.

Rais wa zamani wa Marekani George W Bush aliongoza kutoa risala za rambi rambi, akisema Marekani “imepoteza mojawapo ya sauti zinazotegemewa na za kipekee kuhusu mambo ya nje”.

Mabinti wa Rais Richard Nixon, Tricia Nixon Cox na Julie Nixon Eisenhower, walisema kwamba hadithi ya maisha ya Kissinger ilikuwa ya kipekee sana – na ya Kimarekani kabisa.

“Henry Kissinger atakumbukwa kwa muda mrefu kwa mafanikio yake mengi katika kuendeleza mambo ya amani,” ilisema taarifa hiyo.”Lakini ilikuwa tabia yake ambayo hatutasahau kamwe.”

Mzaliwa wa Bavaria mwaka wa 1923, mtoto wa mwalimu wa shule alikuja Marekani kwa mara ya kwanza mwaka wa 1938 wakati familia yake ilikimbia Ujerumani iliyotawaliwa na Wanazi.

Dkt. Tulia atoa maagizo kwa Kamati ya IPU
Benchikha anataka makombe Simba SC