Beki wa pembeni wa Man City Benjamin Mendy ataendelea kuwa nje ya uwanja kufuatia majeraha ya goti yanayomkabili.
Man City wametoa taarifa rasmi za kuendelea kumkosa beki huyo kutoka nchini Ufarannsa, baada ya kufanyiwa vipimo na kuonyesha bado anahitaji muda zaidi wa kuendelea kupatiwa matibabu.
Meneja wa Man City Pep Guardiola amesema beki huyo atasafiri hadi mjini Barcelona kwa ajili ya matibabu zaidi.
“Kesho anatarajia kwenda Barcelona, tunaamini akiwa huko atapata matibabu ambayo yatamuwezesha kurejea katika hali yake, na kurudi uwanjani kwa haraka zaidi,” amesema Pep Guardiola.
“Hali ya Mendy inamchanganya kila mmoja wetu, lakini hatuna budi kukubaliana na kinachomkabilikwa sasa, natambua anapita katika kipindi kigumu cha kuuguza jereha la goti, lakini bado ninasisitiza, sina shaka kabisa, kwani ninatarajia kumuona tena akicheza msimu huu.
“Kwa sasa tuna wachezaji wenye uwezo wa kucheza nafasi ya beki wa pembeni kama Danilo, Fabian Delph, Fernandinho, na hata kiungo Oleksandr Zinchenko ana uwezo huo.” Aliongeza kocha huyo kutoka Hispania.
-
Real Madrid, Man City zang’ara UEFA Liverpool yabanwa
-
Video: Harry Kane apiga hat-trick ya kwanza klabu bingwa Ulaya
Mendy, alikua na mwanzo mzuri katika kikosi cha Man City baasa ya kusajiliwa akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Ufaransa AS Monaco kwa ada ya Pauni milioni 52.