Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini – TARURA, umesema umejenga madaraja 163 ya mawe yenye thamani ya Shilingi bilioni 8.7 nchini hadi kufikia Machi, 2023 na kupunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 50 huku Shilingi 858.517 bilioni zikiidhinishwa kwa ajili ya Ujenzi, Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya barabara za Wilaya.

Akizungumza na Waandishi wa Habari hii leo Agosti 24, 20223 jijini Dodoma, Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor seif amesema Madaraja hayo yamejengwa katika mikoa ya Kigoma 92, Singida 24, Tabora 5, Kilimanjaro 10, Mbeya 2, Arusha 6, Mrorgoro 2, Rukwa 3, Pwani 1, Ruvuma 3 na Iringa 15.

Ujenzi wa Daraja. Picha ya Lori Van Buren/Times Union.

Amesema kwa mwaka wa fedha 2023/24 jumla ya Barabara zenye km 21,057.06 zitafanyiwa matengenezo, km 427 zitajengwa kwa kiwango cha lami, km 8,775.62 zitajengwa kwa kiwango cha changarawe, madaraja na makalavati 855 yatajengwa na mifereji ya mvua km 70.

“Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 710.31 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 148.207 ni fedha za nje kupitia miradi ya RISE, TACTIC, Bonde la mto Msimbazi na Mradi wa Agri connect na kipaumbele cha TARURA ni kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi,” amesema Mhandisi Seif.

CCM Pwani yawafunda Makatibu wake ushindi wa kishindo
Rais Samia, Rais Xi Jinping wateta nje ya BRICS