Meneja wa TARURA mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Geofrey Mkinga amepewa siku 30 kufanya upembuzi yakinifu wa barabara Suca – Golani katika halmashauri ya Manspaa ya Ubungo yenye urefu wa kilometa 7.5 ili itengewe bajeti na kujengwa kwa kiwango cha lami.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Innocent Bashungwa wakati wa ziara katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kukagua barabara ya Suca – Gorani inayohudumia kata mbili ya Saranga (Jimbo la Kibamba) na Kata ya Kimara (Jimbo la Ubungo).

Bashungwa amesema baada ya Rais Samia Suluhu Hasaan kusikia kilio cha muda mrefu cha mawasiliano barabara hiyo amemuagiza kufika katika eneo hilo na kuhakikisha anatatua kero hiyo ya wananchi.

Waziri Bashungwa amemuagia Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kupitia asilimi 60 ya mapato ya ndani inayotengwa kutekeleza miradi ya maendeleo na asilimi 10 kati ya hiyo inayotengwa kwa ajili ya barabara kulingana na Mwongozo wa Ofisi ya Rais TAMISEMI atenge fedha ambazo atashirikiana na TARURA ili kujenga barabara hiyo.

Wachimbaji wadogo wa madini wakiri kutoelewa sheria za madini
TBS yatakiwa kukamilisha ujenzi kituo cha ukaguzi wa magari bandarini