Chama cha National Unity Platform (NUP) kinachoongozwa na Robert Kyagulanyi ‘Bobi Wine’, kimekishinda mbali Chama cha Rais Yoweri Museveni cha National Resistance Movement (NRM) katika chaguzi za Kampala Capital City Authority (KCCA).
Kwa mujibu wa Gazeti la The Independent, NUP kilishinda viti 41 dhidi ya 44 vya umeya na hivyo kukiacha mbali chama tawala.
Viti vitatu vilivyosalia vilichukuliwa na chama kinachohusiana na mgombea wa zamani wa Urais, Kizza Besigye cha Forum for Democratic Change (FDC).
Hii ni mara ya kwanza katika historia kwa chama kinachoongozwa na Rais Museveni, NRM na Democratic Party (DP) kushindwa katika uchaguzi wa Umeya Kampala.
Chama cha Bobi Wine pia kilishinda viti vyote vya Ubunge kando na kiti cha Kampala ambacho kilitwaliwa na Mohamed Nsereko ambaye alikuwa mgombea huru.