Wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano akiwa nchini Canada kushughulikia suala la ndege aina ya Bombardier Q400, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Justin Trudeau amesema kuwa hawezi kuingilia suala hilo kwakuwa tayari liko mahakamani, hivyo hawezi kuingilia uhuru wa mahakama ambayo anaamini itatenda haki.

Aidha, kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye alipoulizwa kuhusu suala hilo amesema kuwa hawezi kulizungumzia kwa sababu waziri mkuu yupo na wao hawajapata taarifa yeyote.

“Naomba utambue kuwa katibu mkuu bado yupo Canada kwa hiyo mambo mengine mimi siyafahamu hadi atakaporudi atujulishe kilichojiri huko Canada,”amesema Nditiye

Akizindua uwanja wa ndege wa mjini Bukoba, Novemba 6, mwaka huu, Rais Dkt. Magufuli alisema kuwa amemuandikia barua waziri mkuu wa Canada kumuomba kuachiwa kwa ndege hiyo na akaongeza kuwa amemtuma mwanasheria mkuu wa serikali, George Masaju kushughulikia suala hilo.

Hata hivyo, ndege hiyo ya Bombardier Q400-8 inashikiliwa kwa amri ya mahakama nchini humo kutokana na shauri lililopo kati ya serikali na kampuni ya Stirling Civil Engineering.

 

RC Geita aagiza ukaguzi wa mapato ufanyike
Video: Ukuaji wa uchumi wa Taifa unaridhisha - Waziri Mkuu