Benki Kuu ya Tanzania BoT imekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Amana Bank Ltd imefungwa hivyo watumishi na wateja wa benki hiyo wanatakiwa kubadili akaunti.

Katika taarifa iliyotolewa na BoT imewataka wateja na watumishi wote wanaotumia benki hiyo kupuuza taarifa hiyo kuwa ni uzushi, na kuwa benki hiyo inaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Aidha, mapema hii leo kulikuwa na taarifa zilizokuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii kuwa benki hiyo imefungwa huku ikiwaelekeza wakuu wa idara mbalimbali kuwasilisha akaunti zao katika ofisi za utumishi.

Hata hivyo, Benki Kuu ya Tanzania, imetoa rai kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kuacha mara moja kusambaza taarifa za uzushi kwakuwa zina madhara makubwa katika jamii na ni kinyume cha sheria ya benki kuu, hivyo kwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua kali.

Mugabe ajitokeza hadharani akiongozwa na jeshi
LIVE KENYA: Hali tete yatawala, Polisi na wananchi wapambana vikali mapokezi ya Raila