Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu leo Ijumaa Aprili 30, 2021 ametangaza kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM), katika mkutano mkuu maalum wa chama hicho tawala mkoani Dodoma.
Nyalandu alijitoa CCM Oktoba 30, 2017 akiwa Mbunge wa Singida Kaskazini na baadaye kujiunga na Chadema ambako alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Kati.
Uamuzi wake wa kurejea CCM ameuchukua ikiwa zimepita siku 1278 tangu akihame chama hicho, Nyalandu pia alijitosa ndani ya Chadema kuomba ridhaa ya chama hicho kumpitisha kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2021, hata hivyo aliangushwa na Tundu Lissu.
“Ninampongeza rais kwa uongozi wako shupavu. Nakushukuru kwa kukubali kunipokea na kunisamehe pamoja na kuniruhusu kurejea chamani.”