Lydia Mollel – Morogoro
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni – BRELA, imekutana na Taasisi za Udhibiti ili kujadili na kutatua changamoto wanazokutana nazo wadau wa Biashara kutokana na mikinzano na miingiliano ya utoaji huduma, ili kuhakikisha wafanyabiashara wa Tanzania hawakumbani na changamoto au ucheleweshwaji wa kupata huduma katika ufanyaji wa biashara hapa nchini.
Akizungumza katika kikao hicho, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni – BRELA, Godfrey Nyaisa amesema tangu kupitishwa kwa mpango wa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini MKUMBI-Bllue Print mwaka 2018 na kuanza utekelezaji wake mwaka 2019, Serikali imefanya juhudi mbalimbali ili kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini.
Amesema, “BRELA ikiwa ni ya utendaji na kusababisha usumbufu kwa wateja pale ambapo Mfanyabishara amepewa kibali cha kufanya biashara na Taasisi ya Udthibiti bila kusajili biashara yake ,na pindi anapotaka kusajili inatokea mfanano wa majina yaliyokwisha kusajiliwa BRELA hivyo inabidi abadili jina husika.”
Aidha, Nyaisa ameongeza kuwa, BRELA inakumbana na changamoto zitokanazo na Sheria zinazosimamia taasisi za udhibiti husika,maelekezo ya kiutendaji na wakati mwingine uelewa mdogo wa baadhi ya watendaji katika Taasisi mbalimbali za udhibiti, kuhusu majukumu na mamlaka ya BRELA wanaposhughulikia na kutoa huduma kwa wateja wao.