Radi iliyoambatana na mvua iliyopiga katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita imesababisha vifo vya ngo’mbe 26 wa wafugaji kutoka kaya sita.

Mtendaji wa kijiji cha Msonga, Andrew Tangu amesema katika tukio hilo wafugaji; Bundala Saliboko, Joseph na Shikome Mlekwa kila mmoja amepoteza ng’ombe sita huku Christopher Aloyce amepoteza ngombe wanne, Cecilia Sengerema Ng’ombe watatu na Ndaki Paul amepoteza ng’ombe mmoja.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Mponjoli Mwambulambo amesema tukio limetokea saa 11:00 jioni ya Machi 3, 2020 wakati mifugo hiyo ikiwa machungani.

Mkuu wa wilaya ya Bukombe, Said Nkumba ametoa salamu za pole kwa wafugaji hao na kutoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwa kuepuka kujikinga mvua chini ya miti mirefu inayovutia radi.

“Nawasihi wananchi kutambua kuwa matukio haya ya radi hayahusiani na imani za kishirikina, nawaonya waganga wa kienyeji na wapigaramli chonganishi kutowagombanisha wananchi kuhusiana na matukio haya” Amesema DC Nkumba.

Rushwa yamtia mbaroni Askari Mgambo
Mbowe atoa sababu kutokualikwa Ikulu