Mwanamuziki nyota kutoka nchini Nigeria Burna Boy amedhihirisha kuguswa na msiba wa rapa ‘AKA’.

Kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta story) Burna Boy amechapisha mashairi yaliyo katika mfumo wa wimbo wa maombolezo ya kifo nyota huyo.

“Haya yote ya nini?, nimesikia amefariki, niliiona video ya kwenye ule mgahawa na ilinitoa katika hali yangu ya kawaida, hii ilinirudisha nyuma hadi siku ile ulipoiona bastola yanguna ukasema nilikuwa mwenye hofu.

Kisha nikakwambia pia, nawe unatakiwa kuwa nayo, Kwa sababu sio kwamba washkaji hawafi lakini nilijua kuwa unafahamu, na kiukweli hatukuwa tunaelewana, lakini sikutaka ufe.

Natumai watamshika yeyote aliyekufanyia ukatili huu, natumai utapumzika kwa amani, hata kama hatukuwa saqa kimaelewano, mwisho wa siku sisi ni watu wazima” ameandika Burna Boy.

kutoka kushoto ni msanii wa Nigeria Burna Boy akiwa na marehemu AKA enzi ya uhai wake

Ikumbukwe Burna Boy na AKA waliwahi kupitia kipindi cha kutokuwa na maelewano mazuri kilichoanzia mnamo mwaka 2019 ambapo rapa AKA alitweet akiwa na hasira baada ya timu ya mpira qa miguu ya Afrika kusini kushindwa na Nigeria kwenye kombe la mataifa ya Afrika nchini Misri.

Tweet hizo zilichochewa na rapa Ycee kutoka Nigeria ambaye alizitumia kama fimbo ya kumchapia AKA kimashairi.

Na baadae uzito wa mzozano baina yao ulichochewa zaidi na machafuko yaliyotokea nchini Afrika Kusini ambao raia qa nchi hiyo walikuwa wakiwafanyia fujo wahamiaji.

Wakati huo Burna boy alionyesha kutoridhishwa na ukimya wa marehemi AKA kama kioo cha jamii na kumtaka asimamie haki na aonyeshe jitihada za kutafuta utatuzi kwa kupaza sauti dhidi ya wananchi wa Afrika ya kusini waliokuwa wakiwabagua wahamiaji nchini humo.

Familia ya marehemu ‘AKA’ yatoa taarifa hii mpya

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 17, 2023
Wizi wa Maandazi: Mwalimu, Mlinzi mbaroni kwa shambulizi