Kiungo kutoka nchini Ecuador Moisés Isaac Caicedo Corozo ameutaka Uongozi wa Klabu ya Brighton & Hove Albion kukubali kumuachia ajiunge na Arsenal FC, katika kipindi hiki cha Usajili wa Dirisha Dogo.
Klabu ya Arsenal jana Ijumaa (Januari 27) ilituma ofa ya Paund Milioni 60 kwa ajili ya kumsajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21, lakini Uongozi wa Brighton & Hove Albion umeripotiwa kuiweka kapuni ofa hiyo.
Mapema leo Jumamosi (Januari 28) Caicedo ametuma ujumbe Brighton & Hove Albion kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akiutaka wakubali kumuachia ili aondoke klabuni hapo katika kipindi hiki.
Caicedo ameandika: “Ninawashukuru Bw. Bloom na Brighton kwa kunipa nafasi ya kuja Ligi Kuu England na nahisi siku zote nimefanya vyema kwa ajili yao. Kila mara nacheza soka kwa tabasamu na kwa moyo.”
“Mimi ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto 10 kutoka katika malezi duni huko Santa Domingo nchini Ecuador. Ndoto yangu daima kuwa mchezaji mashuhuri zaidi katika historia ya Ecuador.”
“Najivunia kuweza kuleta ada ya rekodi ya uhamisho kwa Brighton ambayo ingewawezesha kuwekeza tena na kusaidia klabu kuendelea kuwa na mafanikio.”
“Mashabiki wameniweka moyoni mwao na daima watakuwa moyoni mwangu hivyo natumai wanaweza kuelewa kwa nini wanataka kuchukua nafasi hii nzuri.”