Chama cha Mapinduzi CCM kimevigalagaza vyama vya upinzani na kuibuka mshindi katika uchaguzi mdogo wa wabunge, kwenye majimbo matatu ya Songea Mjini, Longido na Singida Kaskazini.
Katika Jimbo la Songea Mjini ambalo liliachwa wazi baada ya mbunge wake, Leonidas Gama kufariki dunia, mgombea wake Dkt. Damas Ndumbaro ametangazwa kuwa mshindi kwa kupata kura 45,762 sawa na 97%, huku mgombea aliyemfuatia wa CUF akiwa amepata kura 608, na mgombea wa ADA-TADEA akiwa wamepata kura 471.
Aidha, Katika jimbo la Singida Kaskazini ambalo liliachwa wazi na Lazaro Nyalandu aliyejiuzulu wadhifa wake, CCM imechukua tena jimbo hilo ambapo msimamizi wa uchaguzi, Rashid Mandoa amemtangaza mgombea Justine Monko (CCM) kuwa mshindi baada ya kupata kura 20,857 sawa na 93.5%.
Kwa upande wa jimbo la Longido msimamizi wa uchaguzi, Jumaa Mhina amemtangaza Dkt. Stephen Kiruswa kuwa mshindi baada ya kupata kura 41,258 sawa na 99.1%.
-
Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema atimkia CCM
-
Musukuma awavaa Chadema, asema hawana ubavu wa kumfukuza Lowassa
-
CCM yatamba kushinda majimbo yote
Hata hivyo, Uchaguzi huo umefanyika jana Januari 13, huku chama kikubwa cha upinzani nchini CHADEMA na CUF ya Maalim Seif, vikiwa vimesusia uchaguzi huo.